Rais wa Urusi Vladimir Putin jana amekutana na rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron, katika kile kinachoonekana kuwa ni hatua muhimu ya kuuweka vizuri uhusiano wao.
Viongozi hao wanatarajiwa kujadili uhusiano kati ya nchi hizo, hususan biashara na ushirikiano, katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Balozi wa Urusi nchini Ufaransa Alexander Orlov, amesema mkutano wa rais Macron na Putin,ni muhimu kwa mataifa hayo.
Viongozi hao pia wanatarajiwa leo kuhudhuria ufunguzi wa maonesho ya Versailles, ya kuadhimisha miaka 300 ya ziara ya mfalme Peter wa Urusi alipozuru Ufaransa.
