Rais wa Uturuki aonya kuwa nchi yake itachukuwa hatua zaidi dhidi ya wapiganaji wa Kikundi nchini Syria na Iraq,

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameonya kuwa nchi yake itachukuwa hatua zaidi dhidi ya wapiganaji wa Kikundi nchini Syria na Iraq, katika wakati ambapo vikosi hivyo vinavyoungwa mkono na Marekani, vikikaribia kukamilisha operesheni ya kuzitwaa ngome za kundi lijiitalo, Dola la Kiislamu, IS.

Akizungumza katika mji mkuu wa nchi yake, Istanbul, hapo jana, Erdogan ameitaka Marekani iwache kuwaunga mkono wapiganaji hao wa Kikurdi, na kwamba hiyo itakuwa ajenda yake kwenye mazungumzo na Rais Donald Trump anayeitembelea Uturuki mwezi huu.

Kauli ya Erdogan ilikuja muda mchache baada ya taarifa za wanamgambo hao wa Kikurdi kulitwaa eneo la Tabqa, mji ulio umbali wa kilomita 40 kutoka yalipo makao makuu ya IS, Raqqa.

Marekani inakichukulia kikosi cha Wakurdi wa Syria, SDF, kama mshirika muhimu wa kupambana na IS kaskazini mwa Syria, lakini Uturuki inakiangalia kikosi hicho kama tawi la vuguvugu la Wakurdi lililomo ndani ya ardhi yake ambalo inalitambua kama kundi la kigaidi.

 

Exit mobile version