Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, amesema serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika samaki visiwani Zanzibar.
Aidha amesema katika kipindi kifupi kijacho, Zanzibar inatarajia kuwa na meli ya uvuvi pamoja na kampuni ya samaki, ili kuwanufaisha wavuvi na Wazanzibari kwa ujumla.
Akizungumzia maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini, amesema serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuimarisha miundombinu, ili kuhimili maafa hayo kwa kuzuia maji yasituame.
Amesema ni matumaini yake baada ya miaka mitatu ijayo, maafa ya mvua yataondoka na kubaki kuwa historia zanzibar.
