Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameikemea Wizara ya Afya kwa kutotekeleza agizo lake la kujengwa na kukamilisha kwa wakati, ujenzi wa Kituo cha Afya Pemba.
Dk Shein alionyesha kutofurahishwa na wizara hiyo kutofanyia kazi agizo lake, katika ziara yake ya kutembelea miradi kisiwani Pemba.
Dk Shein hakuridhishwa na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Ngomeni, kutokana na kutokamilika licha ya agizo lake la Novemba mwaka jana.
Kutokana na hali hiyo ameagiza tena Wizara ya Afya kuhakikisha wanafanya kazi kwa uhakika, na kukamilisha ujenzi huo ndani ya miezi mitatu.
