Rappa Eminem ndani ya bifu zito na Channel ya TV ya REVOLT

Rappa Eminem au kwa jina lake halisia Marshall Mathers (47), aingia
katika bifu na Channel ya TV ya REVOLT, hii ni baada ya nakala
original ya wimbo wake wa bang alioimba na Conway kuvujishwa,
ambapo katika nakala hii ambayo imesemekana kuwa nakala ya
kwanza ambayo ilirekodiwa, baadhi ya mistari iliikashifu Televisheni
hii inayomilikiwa na P Diddy, ambapo alisema , ‘Yeah shout out to
Puffy Combs, but Fk Revolt’. Sasa ugomvi huu umeunganishwa na ugomvi kati ya Eminem na Joe Budden, ambae pia ni mtangazaji wa stesheni hio ya TV inayomilikiwa na P Diddy. Sasa baada ya nakala hii ambayo ikotofauti na nakala ilioachiliwa mwaka jana mwezi wa saba kuvujishwa, REVOLT walijibu kwa kupost picha katika kurasa wao wa twitter Fk Eminem.

Exit mobile version