Ikiwa imepita siku moja tangu kuelezwa kwa adha ya usafiri wa
mabasi yaendayo kasi kituo cha Kimara jijini Dar es Salaam,leo
Alhamisi Oktoba 12 Mkuu wa Mkoa wa huo Albert Chalamila
ametembelea kituo hiko na kusikiliza kero za wananchi.
Hali ya idadi ya watu katika kituo hicho leo ni tofauti na jana,
ambapo msongamano ulikuwa mkubwa huku wakala wa Mabasi
hayo (Dart) wakikiri kuwapo kwa kadhia hiyo na wakieleza
namna ya kutatua ikiwa moja ya njia hizo ni kuongeza mabasi
hayo.
