Mkuu wa Mkoa DSM wa Paul Makonda leo July 9 amezungumza na Mkuu wa Wilaya mpya wa Temeke Mh Godwin Gondwe pamoja na DC mstaafu Temeke FelixLyaniva
Mh Makonda amemwambia mstaafu Felix Lyaniva kuwa alikuwa mtu mwema sana na anajua watu wa temeke wata-mmisi kama kustaafu basi amestaafu vizuri sababu ameacha mafaniko mengi Temeke.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya mpya Mh Godwin Godwe amekaribishwa na Mkuu wa Mkoa Mh Makonda na kuambiwa ahakikishe anafuatilia vyema Wilaya yake ya Temeke maana ni kubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh Godwin Gondwe amehaidi kutekeleza yale yote aliyoambiwa na Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda ili kuleta maendeleo Zaidi Temeke.
