Zaidi ya watu milioni 200 duniani kote hawana ajira, ikiwa ni ongezeko kwa asilimia 3.4 kutoka mwaka jana.
Shirika la kazi duniani ILO limetoa takwimu hizo katika ripoti yake ya jana, ikisema chanzo kikubwa ni kudorora kwa biashara za kampuni ndogo na za kati SME.
Ripoti hiyo inasema kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni nchi maskini, ambako biashara ndogo na za kati ndio vichocheo vinavyotegemewa zaidi, kwenye ajira na kukuza uchumi.
Kwa nchi za kiarabu asilimia 70 za ajira ni kwenye kampuni hizo, ilhali kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, kampuni hizo hutegemewa katika kuajiri asilimia 50 ya nguvukazi.
Takwimu kutoka zaidi ya nchi 130 zinaonyesha kuwa, biashara ndogo na za kati zilikuwa na ukuaji mkubwa kabla ya mdororo wa kiuchumi mwaka 2008.
Hata hivyo kuanzia mwaka 2009 hakukuwepo na ongezeko la ajira katika sekta hiyo, jambo linalochagiza umuhimu
