Ripoti ya Tanzanite, Almas yawatafuna Mawaziri.

In Kitaifa

Leo rais Dk John Pombe Magufuli amepokea ripoti za uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Ripoti hizo zimetokana na kamati mbili zilizoundwa na spika wa Bunge Job Ndugai.

Katika maelezo yake kabla ya kumkabidhi Rais ripoti hizo, Waziri mkuu Majaliwa amesema kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakilalamika serikali kutowajali na kuwasikiliza.

Antenna imeinasa sehemu ya ripoti hiyo kama ilivyokuwa ikiwasilishwa na mwenyekiti wa kamati husika mheshimiwa Azzan Mussa Zungu.

Mara baada ya kupokea ripoti hizo, Rais Magufuli amechukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa wateule wote waliotajwa katika ripoti hizo.

Miongoni mwa wateule wa Rais waliotajwa katika ripoti hiyo ni pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Edwin Ngonyani.

Wengine waliotajwa katika taarifa hizo ni pamoja na Katibu Tawala Eliakim maswi, wabunge Willium Ngeeleja na Endrew Chenge.

Muda mfupi baada ya agizo hili la mheshimiwa rais, Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ameripotiwa kuandika barua ya kujiuzulu baada ya jina lake kutajwa katika uchunguzi huo.

Nae naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani, amesema anaandika barua ya kujiuzulu baada ya Rais John Magufuli kuwataka watu wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo kujiondoa wenyewe.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi Wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu