RPC Geita kathibitisha kukamatwa kwa Mh. Musukuma.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia Mbunge na Mwenyekiti wa CCM Geita, Joseph Musukuma baada ya kukamatwa September 17, 2017 na baadhi ya Madiwani wa Mkoa huo.

Kamanda Mponjoli Mwabulambo amesema bado Mbunge Musukuma na wenzie na wanafanyiwa mahojiano juu ya kilichotokea huku akisema idadi ya watu wenye makosa ikiongezeka.

Na kwa upande mwingine Kamanda Mponjoli amesema Mh.Musukuma alikamatwa na Polisi na sio kuwa aliripoti Kituoni kwa hiari yake kama habari zilivyosambaaya kuwa Mh.Musukuma aliripoti kwa hiari yake.

Lakini pia Kamnda Mponjoli amethibitisha ya kuwa Mh.Musukuma amepelekwa Mahakamani asubuhi ya leo

Kama ulikua ufahamu kuhusiana na ishu hii ya kukamatwa na kupelekwa Mahakamani kwa Mbunge Musukuma ni kwamba;

Mbunge Musukuma pamoja na baadhi ya wadiwani na wananchi, walikamatwa na polisi kwa kufunga njia inayoeleka kwenye mgodi wa GGM na kuleta vurugu, kushinikiza mgodi huo kulipa dola milioni 12.

Exit mobile version