Rufani ya Lema na Mkewe Neema yashindikana kusikilizwa.

Rufani ya Mbunge wa Arusha Mjini Chadema Godbless Lema, na mkewe Neema katika kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo, imeshindikana kusikilizwa jana na kuahirishwa hadi Septemba 19.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda hiyo Angelo Rumisha amesema kuwa, sababu za kuahirisha kwa rufaa hiyo ni kutokana na Jaji Salma aliyepangwa kuisikiliza kuwa likizo.

Lema na Neema wanakipinga kesi ya kudaiwa kumtukana Gambo isisikilizwe na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, kwa kuwa wameshtakiwa kwa sheria ya makampuni wakati wao siyo kampuni.

Wakati kesi hiyo ikiahirishwa Lema ambaye anahudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma,hakuwepo mahakamani hapo

Exit mobile version