Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwa
mauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga
Joachim Mwakyolo yaliyotokea Januari 20 mwaka huu katika
Kijiji cha Kibole kilichopo Kata ya Itete wilayani Rungwe.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Benjamin Kuzaga, ametaja
chanzo cha mauaji hayo kuwa ni mgogoro wa ardhi hekari 60
ambazo marehemu alinunua kwa wenyeji wakati wenyeji
wanadai kuwa eneo hilo ni Hifadhi ya Msitu wa Kijiji cha
Kibole.