SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

In Kitaifa

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya, amefikishwa tena katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambayo leo Jumatatu Februari 20, 2023 imepanga kutaja rufaa ya kupinga hukumu iliyomwachia huru yeye na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Rufaa hiyo namba 155/2022 mbali na Sabaya wajibu rufaa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya huku rufaa hiyo kusikilizwa kwa siku tano mfululizo.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Februari 20, 2023 saa 3:40 asubuhi.

Januari 17, 2023 akiahirisha rufaa hiyo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Judith Kamala, amesema rufaa hiyo itasikilizwa kwa siku tano mfululizo kuanzia Februari 27 hadi Machi 3,2023.

Rufaa hiyo inasikilizwa na Jaji Salma ambaye Desemba 14, 2022 aliahirisha rufaa hiyo na kutoa amri kwa Naibu Msajili huyo, kuchapisha kwenye magazeti tangazo la hati ya wito kwa wajibu rufaa wanne kwenye rufaa hiyo ambao hawakuwepo mahakamani hapo ambao ni Mnkeni, Aweyo, Macha na Msuya.

Rufaa hiyo dhidi ya Sabaya na wenzake watano inapinga hukumu iliyotolewa Juni 10, 2022 na Hakimu Mkazi Patricia Kisinda wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, hukumu iliyowaachia Sabaya na wenzake sita waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  namba 27/2021 katika mahakama hiyo ya chini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu