Sakata la vyeti feki lazua taharuki

Sakata la vyeti feki vya kielimu na taaluma kwa watumishi wa umma, limezua taharuki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada ya kubainika kuwapo kwa watumishi 134 wasio na sifa.
Imeelezwa kuwa wengi wa watumishi hao, wamenaswa katika Idara ya Dharura na wodi zikiwamo za Wazazi na Mwaisela.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof Lawrance Museru, wafanyakazi hao waliokutwa na vyeti feki, wametakiwa kuondoka sehemu zao za kazi mara moja kuanzia jana.
Taarifa hiyo imeonyesha eneo lililoathirika zaidi kwa watumishi wake wengi kubainika wamefoji vyeti, ni wa Idara ya Dharura ya Utoaji Dawa ambayo watumishi 20 wamenaswa na kutakiwa kuondoka.

Exit mobile version