Sakaya amjibu kubenea.

In Kitaifa

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Bara anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Magdalena Sakaya, amejibu mapigo baada ya mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kutangaza jana ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’.

Kubenea amedai kuwa oparesheni hiyo inalenga kumuondoa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Akijibu mpango huo uliotangazwa na Chadema inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Sakaya ambaye ni kambi ya Profesa Lipumba alisema kuwa anawasikitikia Chadema kwa kuingilia mgogoro usiowahusu.

Sakaya ameongeza kuwa Mpango huo wa Chadema hautafanikiwa kamwe na kwamba wanachokifanya  ni  Kuingilia mambo yasiyowahusu.

Katika hatua nyingine, Kubenea alipozungumzia majibu ya Sakaya amedai kuwa CUF ni sehemu ya Ukawa, hivyo inapoonekana inataka kudhoofishwa ina maana kuwa Ukawa itadhoofika pia, hivyo hawako tayari kuliona hilo.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu