Samia Suluhu awahimiza wananchi kudumisha na kuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

In Kitaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na Zanzibar, na kuwahakikishia wananchi wa pande mbili kuwa kero chache za Muungano ambazo zimebaki ,zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya kudumisha Muungano huo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan , ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Mahojiano na vyombo Mbalimbali vya habari, katika kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Aidha,Amesema hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa kwamba unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.

Kuhusu elimu ya Muungano kwa Vijana, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande zote Mbili kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.

Amesema kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu