Saudia ndio mfadhili mkuu wa watu wenye misimamo mikali ya kidini nchini Uingereza kulingana na ripoti mpya.
Ripoti hiyo ya Henry Jackson Society imesema kuwa, kuna ushirikiano wa wazi kati ya mashirika ya Kiislamu, yanayotoa ufadhili kwa wahubiri wenye chuki na makundi ya kijihad yanayokuza ghasia.
Idara ya maswala ya kigeni ilitaka kuchunguzwa kwa jukumu la Saudia na mataifa mengine ya Ghuba.
Ubalozi wa Saudia nchini Uingereza umesema kuwa, madai hayo ni ya uongo dhidi yao.
