Serikali imesema asilimia 61 ya eneo la nchi lipo katika hatari ya kugeuka jangwa ambapo kuwepo kwa hali hiyo imesababisha baadhi ya mikoa kuathirika ikiweno vifo vya mifugo na Wanyama pamoja na kukauka kwa vya nzo vya maji.

Serikali imesema asilimia 61 ya eneo la nchi lipo katika hatari ya kugeuka jangwa ambapo kuwepo kwa hali hiyo imesababisha baadhi ya mikoa kuathirika ikiweno vifo vya mifugo na Wanyama pamoja na kukauka kwa vya nzo vya maji.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba wakati  akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika kesho Mjini Dodoma.
Makamba amebainisha kuwa kuenea kwa hali hiyo ya jangwa na ukame kuna madhara makubwa sana katika uchumi wa Taifa la Tanzania ambapo asilimia80ya watanzania wanategemea kilimo ambacho kwa kiwango kikubwa kinategemea mvua hivyo uzalishaji utapungua.
Aidha amefafanua kuwa  hali  hiyo ya jangwa na ukame ni dhahiri kuwa uzalishaji wa mazao unapungua kwa kiasi kikubwa ikiwemo kupungua kwa upatikanaji wa kipato katika ngazi ya kaya na ngazi ya kitaifa kwa ujumla.
Pia hali hiyo imesababisha upotevu wa rasilimali zingine kama misitu,vifo vya wanayama pori ambao ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni kupitia utalii.
Hata hivyo  Waziri MAKAMBA ameeleza hatua mbalimbali ambazo Serikali imezianadaa katika kukabiliana na jangwa ikiwemo kuandaa taarifa ya hali ya kuenea kwa jangwa na ukame,kutunza na kuhifadhi maliasili pia mkakati kwa Taifa wa kupanda na kutunza miti.
 Waziri huyo ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo isemayo siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame ili kuhakikisha ardhi yetu inatunzwa, kwaajili ya Kizazi cha sasa na Vijavyo.
Exit mobile version