Serikali imewasilisha bungeni bajeti ya shilingi trilioni 31.7, ikiwa imeongeza ushuru wa bidhaa kwa sigara, bia na pombe kali, huku ikipunguza bei za mvinyo na kufuta ada ya mwaka ya leseni za magari na kodi hiyo kuhamishiwa kwenye mafuta ya petroli na dizeli.

In Kitaifa

Serikali imewasilisha bungeni bajeti ya shilingi trilioni 31.7, ikiwa imeongeza ushuru wa bidhaa kwa sigara, bia na pombe kali, huku ikipunguza bei za mvinyo na kufuta ada ya mwaka ya leseni za magari na kodi hiyo kuhamishiwa kwenye mafuta ya petroli na dizeli.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha, kwa mwaka 2017/2018, waziri wa fedha na mipango, dk. Philip Mpango amependekeza pia kufanya marekebisho kwenye sheria ya kodi ya ongezeko la thamani, kwa kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa za mtaji, kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango sifuri katika huduma zinazotolewa kwenye usafarishaji wa bidhaa na mizigo nje ya nchi, na kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vyakula vya mifugo, vinavyotengenezwa nchini.

Pamoja na mambo mengine, Waziri huyo wa fedha, ameliambia bunge juu ya kuchukua hatua za kisheria na kiutawala, ambapo serikali itawatambua rasmi wafanyabiashara wadogo wadogo na wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi, pamoja na kutoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi, huku ikianzisha maeneo maalum (clearing houses) katika viwanja vya kimataifa, migodini na kutozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo.

Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi, Waziri Mpango alifahamisha kuwa Serikali imetenga asilimia 38 ya bajeti yote katika kugharimia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mpango wa taifa wa mwaka 2017/2018, huku kipaumbele kikiwa ni ujenzi wa reli ya kati (standard gauge), kuhuisha shirika la ndege Tanzania, miradi ya chuma liganda na makaa ya mawe mchuchuma na uanzishwaji na uendelezwaji wa kanda maalum za kiuchumi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu