Waajiri katika Taasisi za umma wametakiwa kuhakikisha wanakuwa na ushindani wa kutosha katika maeneo yao ya kazi ili kuleta ushindani hata kwa wafanyakazi hapa nchini, kwani kwa kufanya hivyo hata sekta binafsi nazo zitafata nyayo hizo.
Hayo yamesemwa na mgeni rasmi wa Tuzo za mwajiriwa bora kwa mwaka 2017 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri, Sera, Bunge, kazi,vijana na wenye Ulemavu Mh Jenista Mhagama katika hafla hiyo jijini Dar Es Salaam.
