Serikali inaifanyia marekebisho Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa kuongeza watalaamu waliobobea katika fani hiyo ili kuandaa vitabu bora.

Serikali inaifanyia marekebisho Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa kuongeza watalaamu waliobobea katika fani hiyo ili kuandaa vitabu bora.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mkakati huo wa Serikali bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi).

Mbatia alimuuliza swali la papo hapo Waziri Mkuu, la nini mkakati wa Serikali katika kuondoa vitabu ambavyo vilionekana kwamba vina makosa.

Waziri Mkuu amesema serikali inashughulikia jambo hilo kwa kuiboresha TEA ambapo tayari Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi analifanyia kazi hilo tangu wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tea amewajibishwa kutokana na vitabu vibovu.

Amesema Serikali imekusudia kuiboresha kwa kutumia wasomi waliobobea katika fani hiyo kutoka vyuo vikuu nchini na katika taasisi nyingine kwenda kwenye taasisi hiyo kuandaa vitabu bora.

Waziri Mkuu alikiri kwamba hapo awali kulitokea tatizo kidogo wa uchapishaji vitabu bora wakati serikali ilipoachia kazi hiyo mtu mmoja mmoja kuandaa vitabu vya kiada na ziada.

Waziri Mkuu amesema sera ni kitu kingine, vitabu vinaandaliwa kutokana na sera, mtaala, silabasi na inapendeleza somo lipi liandaliwe katika vitabu gani vya msingi na vya kiada na ziada.

 

Exit mobile version