Serikali inakusudia kutangaza haraka nafasi za ajira katika sekta ya afya baada ya baadhi ya wafanyakazi wake kuacha kazi

In Kitaifa

Serikali inakusudia kutangaza haraka nafasi za ajira katika sekta ya afya baada ya  baadhi ya wafanyakazi wake kuacha kazi ,kutokana na kuwa na vyeti feki na kusababisha zahanati na vituo  vya  afya  kuanza kufungwa kwa kukosa watumishi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amebainisha hayo, kwenye maadhimisho ya siku ya waaguzi duniania yalioyofanyika  Kitaifa katika mji wa Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Waziri Mwalimu amesema kuwa suala la vyeti feki limewakumba zaidi wauguzi na  tayari  Rais John Magufuli ,ametoa kibali cha kuajiri wengine ili kuwazesha wananchi kuendelea kupata huduma katika sekta ya afya.

Amefafanua kuwa  suala hilo litakwenda sanjari na  ajira nyingine  za kawaida, ili kupunguza uhaba  wa watumishi katika sekta hiyo.

Awali katika taarifa  zao  Katibu wa Chama Cha  Wauguzi  Nchini Sebastian Luziga na Rais wake Paul Magesa ,wametaka kutatuliwa kwa changamoto za ukosefu wa dawa, vifaa tiba na maslahi kwa watumishi.

Hivi  Karibuni Rais Dr John Magufuli alitangaza kuwafukuza kazi watumishi wa   umma zaidi ya 9,000 kutokana na kuwa na vyeti feki.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu