Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Libya, imepinga kuachiliwa kwa mwana wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Gaddafi.

Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Libya, imepinga kuachiliwa kwa mwana wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Gaddafi.

Seif Al Islam Gaddafi, alikuwa amezuiliwa na kundi la wanamgambo katika mji ulio magharibi wa Zintan.

Amekaa gerezani kwa muda wa miaka 6 kufuatia mapinduzi yaliyomundoa madarakani babake mwaka 2011, na aliachiliwa baada ya kupewa msamaha.

Kuachiliwa kwa Bwana Al Seif Al Islam huenda kukazua msukosuko zaidi katika nchi hiyo ambayo tayari imegawanyika.

Kwa wale waliokusanyika Tripoli miaka 6 iliyopita kuitisha uhuru, itakuwa ni kama hujuma kwao.

Lakini wengi wa wale waliohojiwa mjini Tripoli walikaribisha kuachiliwa kwa Seif Al Islam.

Exit mobile version