Serikali ipo tayari kumtibu Tundu Lissu.

Dar es Salaam. Serikali imesema ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza hayo leo Alhamis kuwa watafanya hivyo pindi watakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa.

Taarifa hiyo ya Ummy imekuja muda mfupi baada ya Mbunge wa  Singida Kaskazini(CCM), Lazaro  Nyalandu akusema kwamba madaktari wa Kenya wamesema Lissu  hawezi kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya kumpatiwa matibabu.

Mbunge Nyalandu ameeleza hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram, Facebook na Twitter  kwamba  mipango ya kumsafirisha  Lissu ambayo walikuwa wanafanya itasimama kwa sasa  kutokana na ushauri wa madaktari hao  ili kuruhusu kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa vinginevyo.

Exit mobile version