Serikali kuajiri watumishi Elfu 4,339 katika wizara ya mambo ya ndani ya Nchi.

   Serikali inatarajia kuajiri watumishi ELFU NNE 4,339 katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka huo wa fedha.
Wakati huo huo, Nchemba alisema Serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi Rufiji ili kukabiliana na uhalifu katika maeneo hayo.
Akizungumzia uhakiki wa silaha ambazo baadhi zimekuwa zikitumika katika uhalifu, waziri huyo alisema hadi kufikia Machi mwaka huu, asilimia 63.2 ya silaha hizo zilikuwa zimehakikiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo, ameiitaka Serikali iimarishe ulinzi katika wilaya za mkuranga, Kibiti na Rufiji ili wananchi wa maeneo hauo waweze k
Exit mobile version