Serikali kujenga daraja la Juu kwaajili ya kivuko cha waenda kwa miguu(Over head Pedestrian Bridge)

     Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandis Edwin Ngonyani ,amesema kuwa Serikali itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu (Over head Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni jijini Dar es salaam.
Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu.
Hata hivyo ameongeza kuwa  Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika Barabara  ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka taa hizo katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote.
Exit mobile version