Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako amesema kwa mwaka
wa fedha 2022/23, serikali inatarajia kujenga Vituo Atamizi vya
kulea ujuzi wa vijana kwenye kanda tano nchini.
Vituo hivyo, vitatoa fursa kwa vijana kufanya mafunzo kwa
vitendo sambamba na kufanya shughuli za uzalishaji mali
kwenye vituo hivyo ili waweze kujiingizia kipato kutokana na
ujuzi watakao kuwa wameupata kwenye vituo hivyo.
Prof Ndalichako ameyasema hayo wakati akizungumza na
wanafunzi wa Vyuo vya ufundi vya Don Bosco na VETA jijini
Dodoma ambao wananufaika na Programu ya Taifa ya kukuza
ujuzi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.
