SERIKALI inakusudia kutangaza haraka nafasi za ajira katika sekta ya afya baada ya baadhi ya wafanyakazi wake kuacha kazi kutokana na kuwa na vyeti feki na kusababisha zahanati na vituo vya afya kuanza kufungwa kwa kukosa watumishi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amebainisha hayo leo kwenye maadhimisho ya siku ya waaguzi duniania yalioyofanyika Kitaifa katika mji wa Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri Mwalimu amesema kuwa suala la vyeti feki limewakumba zaidi wauguzi na tayari Rais John Magufuli ametoa kibali cha kuajiri wengine ili kuwazesha wananchi kuendelea kupata huduma katika sekta ya afya.
Amefafanua kuwa suala hilo litakwenda sanjari na ajira nyingine za kawaida ili kupunguza uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.
Awali katika taarifa zao Katibu wa Chama Cha Wauguzi Nchini Sebastian Luziga na Rais wake Paul Magesa wametaka kutatuliwa kwa changamoto za ukosefu wa dawa, vifaa tiba na maslahi kwa watumishi.
Hivi Karibuni Rais Dr John Magufuli alitangaza kuwafukuza kazi watumishi wa umma zaidi ya 9,000 kutokana na kuwa na vyeti feki
