Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikali
itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi ya
Zanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na Asasi nyingine
katika uwezeshaji wananchi kiuchumi, ulinzi wa watoto dhidi ya
vitendo vya udhalilishaji ikiwemo uimarishaji lishe kwa watoto.

Dkt Mwinyi ameyasema hayo katika maadhimisho ya mwaka
mmoja tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo,na kueleza kuwa
anaridhishwa na hatua zinazochukuliwa katika kuwakomboa
wananchi, hasa wanawake wanaojihusisha na kilimo.

Exit mobile version