Serikali kuwasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii

Serikali inatarajia kuwasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii, yatakayoanzisha fao la upotevu wa ajira.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Ajira Anthony Mavunde, ametoa kauli hiyo leo bungeni alipojibu swali la Mbunge wa Busega CCM Dk Raphael Chegeni.

Mbunge huyo alitaka kupata tamko la Serikali kuhusu uwezekano wa kuunganishwa mifuko ya hifadhi ya jamii, na kuondoa mkanganyiko kwa wanachama.

Naibu waziri amesema Serikali imeandaa mapendekezo ya kuunganisha mifuko mitano inayotoa mafao ya pensheni, na kubaki na michache ambayo ni imara.

Exit mobile version