Serikali Mkoani Kilimanjaro imeliagiza Jeshi la Polisi Mkoani hapo, kufanya ukaguzi maalumu wa magari yanayobeba wanafunzi hususani shule binafsi ,ili kujiridhisha kama yana sifa ya kufanya kazi hiyo.
Mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecki Sadiki amesema hayo wakati wa Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) ,ambacho kilikuwa maalumu kwa suala la hifadhi ya mazingiraambapo amekitaka Kikosi cha usalama barabarani kiandae mpango wa ukaguzi wa magari ya wanafunzi kila Jumamosi, na yale yasiyo na sifa yaondolewe barabarani.
Sadiki amesema Serikali ilisikitishwa na vifo vya watu wasio na hatia ,kwani pia katika ajali hiyo mkoa wake uliguswa kwa kupoteza watoto 14.
Aidha amemtaka Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issa kusimamia kikamilifu ukaguzi huo ili kuepuka udanganyifu.
