Serikali mkoani Kilimanjaro yaanza rasmi zoezi la kukagua magari yanayo safirisha wanafunzi.

   Serikali mkoani Kilimanjaro imeanza zoezi rasmi la operesheni maalumu ya kukagua magari yanayosafirisha wanafunzi wa shule za mkoa huo ili kujiridhisha kama yana ubora ambao unastahili katika kutoa huduma  ambayo ni salama na bora kama yalivyo maelekezo ya sheria za usafirishaji.
Akizungumza na vyombo vya habari  mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadiki amesema katika kuhakikisha zoezi hilo linatekelezwa ipasavyo,wameshirikisha jeshi la polisi ,temesa na mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu(Sumatra) na kwamba litafanyika kila jumaosi na jumapili,ili kutoathi masomo kwa wanafunzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah amesema katika zoezi hilo wanakagua ,uzima wa gari,ikiwemo ,rangi,mikanda,viti na mfumo wa breki,na kwamba wanapogundua gari lenye ubovu,wana liondoa namba zake,kisha kumwagiza mmiliki wake akalitengeneze ndipo aruhusiwe kuendelea na usafirishaj.
Nae afisa wa mfawidhi wa Sumatra mkoani Kilimanjaro Johns Makwale,amesema licha ya wamiliki kuwa na nyaraka muhimu za kuwaruhusu kufanya biashara ya usafirishaji ,baadhi ya magari yamegundulika kuwa na kasoro ndogo ndogo,ikiwemo uchakavu wa viti pamoja na kutokupigwa rangi iliyopendekezwa.
Exit mobile version