Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha miradi mikubwa inatekelezwa kama ilivyoaidiwa.

Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh.dkt John Magufuli amewahakikishia wananchi wa mkoa wa pwani kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla linatekelezwa kama ilivyoahidi.
Mh Raisi John magufuli amesema hayo katika mkutano wa hadhara uluofanyika katika uwanja wa bwawani mjini kibaha akiwa katika ziara ya kwanza katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani pwani.
Dkt Magufuli ameitaja miradi hiyo ikiwa ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa(standard gauge)ambayo imeanzwa kujengwa,ujenzi wa barabara ya njia sita kati ya dar-es-salaam na chalinze yenye urefu wa kilomita 128,ujenzi wa bandari kavu ya ruvu itakayo pokea mizigo kutoka katika banadari ya dar-es-salaamu na ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko yam to rufiji amabo mipango ya kushirikiana na Ethopia imeanza.
Amebainisha pamoja na kutekeleza miradi hiyo serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watu  waliohujumu taifa ikiwemo kujihusisha na vitendo vya wizi na rushwa,na aitakatishwa tama na watu wanao lalamika na  wanaobeza juhudi hizo.
Mapema akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa wa pwani,mkuu wa mkoa mhuhandisi Evarest ndikilo amesema kuwa mkoa huo unajumla ya viwanda 371 ikiwemo viwanda 9 vikubwa  na kwamaba ujenzi wa viwanda hivyo unaendelea katika hatua mbali mbali.
Exit mobile version