Serikali ya Morocco yakubaliana haya na Tanzania

Serikali ya Morocco imesema kuwa iko tayari kushirikiana na Tanzania katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanano na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwekeza kati mradi mkubwa wa Nishati ya jua.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Morocco hapa nchini, Benryane Abdelilah Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amesema kuwa Morocco ipo tayari kuwekeza katika mradi mkubwa wa Nishati ya Jua ‘Solar energy’, ili kuweza kusaidiana na Tanzania katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema kuwa Idara ya Mazingira inatakiwa kuainisha maeneo ya vipaumbele kwa upande wa mazingira na kusema  kuwa, mradi huo mkubwa wa uzalishaji wa  Nishati ya jua utakaotekelezwa na kampuni kutoka Morocco ya Masen Campany Limited,

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amesema kuwa kabla ya uwekezaji wa mradi mkubwa wa aina hiyo, inatakiwa ifanyike tathmini ya athari ya mazingira na kuahidi kuwa watakapokuwa tayari zoezi hilo litafanyika kwa haraka.

Hata hivyo, Balozi Benryane Abdelilah amesema kuwa utatuzi wa tatizo hilo la mabadiliko ya tabianchi utasaidia kuokoa kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira hapa nchini.

Exit mobile version