Serikali ya Tanzania yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra.

In Kitaifa, Uchumi

Shughuli zimeanza tena katika mgodi mkubwa zaidi wa madini ya almasi nchini Tanzania, licha ya mzozo na serikali ya Tanzania, ambayo ilikamata bahasha iliyokuwa na almasi kwenye uwanja wa ndege.

Shughuli katika mgodi wa Williamson zimerejeshwa baada ya kusimamishwa kwa siku nne.

Wiki moja iliyopita hisa kwenye kampuni ya Uingereza ya Petra zilishuka kwa asilimia 7, baada ya almasi zake kuzuiwa kusafirishwa kutoka nchi Tanzania, ambapo pia wafanyakazi wake kadha walihojiwa na mamlaka za nchi hiyo.

Mamlaka zilikamata bahasha iliyokuwa na almasi ambayo hadi sasa haijaachiliwa.

Mazungumzo ya kampuni na serikali kuhusu suala hilo yanaendelea, kwa kujibu wa kampuni ya Petra.

Kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuchimba almasi nchi Tanzania inalaumiwa kwa kuzusha thamani ya almasi zake.

Serikali inasema kuwa Petra iliandika mzigo huo kuwa wa thamani ya dola milioni 14.6 wakati thahamia yake halisi ilikuwa dola milioni 29.5.

Petro ilikana madai hayo, ikisema kuwa serikali ndiyo inahusika kwa kuthibitisha thamani kama hiyo.

Mgodi wa Williamson ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania unamilikiwa na Perto kwa asilimia 25 huku serikali ya Tanzania ikimiliki asilimia 25.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu