Serikali ya Venezuela imesema kuwa,nchi hiyo inakabiliwa na ongezeko kubwa la vifo vya watoto na akina mama.
Wizara ya Afya imesema idadi ya wanawake wanaofariki wakati wa kujifungua imeongezeka kwa asilimia 65, na idadi ya watoto wanaofariki wanapozaliwa imefikia asilimia 30.
Imeelezwa pia kuwa kumekuwa na ongezeko la magoinjwa ya malaria na Donda koo.
Venezuela imekuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa takriban dawa zote, katika vitengo vyake vya Afya.
