Serikali ya Zambia inapanga kutupilia mbali kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini humo, na kumuachilia huru kutoka jela hii leo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia maafikiano, ambayo yamefikiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na wanasheria.
Hakainde Hichilema ambaye ni kiongozi wa chama cha Umoja wa Maendeleo ya Taifa UPND pamoja na wengine watano, walikamatwa mwezi Aprili na wakashitakiwa kwa kosa la uhaini.
Kesi dhidi ya Hichilema ilipaswa kuanza kusikilizwa leo, lakini vyanzo vya habari vimesema mwendesha mashtaka atawasilisha ombi la kesi hiyo kutupiliwa mbali.
