SERIKALI YAAGIZWA KUFUTWA KWA LESENI 73.

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeielekeza Tume ya Madini kufuta jumla ya leseni 73ambazo maeneo yake hayajaendelezwa.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Madini,ANTHONY MAVUNDE wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu baadhi ya Wamiliki wa leseni ambao wanahodhi maeneo bila kufuata Sheria.

Aidha, MAVUNDE amefafanua leseni hizo ambazo zinafutwa ni wamiliki wa Leseni za utafutaji wa madini 44 ambao wameshindwa kurekebisha makosa yao huku wamiliki wa leseni 29 za uchimbaji wa kati wa madini wameshindwa kurekebisha makosa yao.

Pia,amefafanua kuwa,kufuatia uwepo wa makosa hayo, Tume ya Madini ilitoa Hati za Makosa kwa jumla ya leseni 205, ambazo zinajumuisha leseni za utafiti wa madini 110, na leseni za uchimbaji mkubwa na Amebainisha kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu lengo ni kuhakikisha wanaokata Leseni wanazifanyia kazi kwa maslahi ya Taifa.

Katika hatua nyingine,Waziri MAVUNDE amesema hatawavumilia watu wanaochukua leseni na kukaa nazo bila kuziendeleza.

Ikubukwe kuwa mnamo Mwezi April Mwaka huu wa 2025 Wizara ya Madini ilitoa tamko la ufutaji leseni ikiwa ni pamoja na kutoa Hati za makosa kwa makampuni mbalimbali hasa makubwa ambapo kwa muda mrefu walikuwa hawajaendeleza maeneo yao na baada ya hapo Makampuni mengi yaliwasilisha taarifa zao za utetezi na mengine yameanza shughuli za uchimbaji.

Exit mobile version