SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa ,Serikali ya Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika huduma za Hali ya hewa ikiwemo ununuzi Wa miundombinu ya kisasa za uchunguzi Wa Hali ya hewa ikiwa ni Pamoja na rada.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu waziri Wa Ujenzi na uchukuzi ATUPELE KIBETE,wakati alipokuwa akizungumza katika siku ya Hali ya hewa Duniani.
Naibu waziri KIBETE, amesema kuwa Wana rada saba ambapo rada tatu zimeshasinikwa katika maeneo tofauti hapa nchini rada mbili zimeshafika na wanategemea kuzifunga hivi karibuni katika Mkoa Wa Mbeya na maeneo ya Kigoma ,na rada zingine mbili zipo kiwandanj zinatengenezwa.
Amesema kuwa,katika kukabiliana na changamoto na athari za mabadililo ya Hali ya hewa, kunahitajika jitihada na hatua za makusudi endelevu ikiwa Pamoja na kujenga taasisi madhubiti Kwa ajili ya kuboresha na kutoa huduma za Hali ya hewa Nchini.
Naibu waziri huyo ,amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 wanachama wa WMO na imeungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha miaka 73 ya WMO na maadhimisho ya miaka 150 ya Shirika la Kwanza la Kimataifa la Hali ya Hewa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, (TMA)Dkt. LADISLAUS CHANG’A, amesema katika ukanda Wa Afrika Mashariki na Dunia mzima Wana changamoto ya mabadililo ya hali ya hewa ambayo zinapelekea kubadilika Kwa misimj ya mvua na upunguvu Wa unueshaji Wa mvua.
Amesema kuwa ,Shirika la Hali ya Hewa Duniani linataka taasisi zote zinazotoa utabiri walau usahihi uwe asilimia 70, kwa Tanzania, usahihi wa utabiri wetu ni asilimia zaidi ya 86, ni nchi ambayo inaheshimika sana kwa ubora wa utabiri na huduma za hali ya hewa duniani.
