Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abass amekutana na kuzungumza na wanahabari asubuhi ya leo kuhusiana na kulifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa muda wa miaka miwili sawa na miezi 24 kutoka na alichokieleza kuwa Gazeti hilo kukiuka misingi na taratibu za Uandishi wa Habari.
Dr.Hassan amezieleza sababu za Serikali kulifungia Gazeti hilo kutokana na ukiukwaji na misingi na sheria pamoja na kanuni za Uandishi wa Habari.
Mwisho Msemaji huyo wa Serikali Bw.Hassan Abbas akatoa wito kwa wanahabari kusimamia weledi ,misingi na kanuni za habari kwani Uandishi wa Habari ni taaluma kamili.
