Serikali yajipanga kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandao.

In Kitaifa
Serikali imesema inajipanga kukabiliana na matumizi mabaya ya mtandao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wanaotumia vibaya.
Akizungumza katika majadiliano ya usalama wa mitandao ya kijamii kati ya Tanzania na China, Naibu Waziri wa Wizara wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Edwin Ngonyani amesema serikali itawachukulia hatua kali wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii, wakiwamo wanaotuma ujumbe wenye dhamira ya kuwachafua wengine.
Injinia Ngonyani amesema kuwa Tanzania bado ipo nyuma sana katika usimamizi wa mitandao ya kijamii tofauti na china mbayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Naibu Waziri wa Udhibiti wa mtandao wa China, Ren Xianliang amesema nchi yao imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kudhibiti matumizi ya usalama wa mtandao, kwa kuwa walianzisha mtandao wao ambao umekua unasaidia kufuatilia masuala ya nchi yao vikiwamo vivutio mbalimbali ambavyo huwashawishi na kutoa hamasa kwa wananchi wengi kuweza kutumia mtandao huo.
Aidha amesema pia china imekuwa ikifanya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari kwa kuandaa vipindi maaalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu