serikali yakanusha taarifa zilizozagaa kuhusu kutenguliwa kwa agizo la Dkt Harison Mwakyembe.

In Kitaifa

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imekanusha taarifa zilizozagaa kuhusu kutenguliwa kwa agizo la Dkt. Harison Mwakyembe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuhusu uchambuzi wa habari za magazeti katika redio na televisheni kuwa ni za uzushi.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa taarifa zilizozagaa, hazina ukweli wowote na Rais Dkt. John Magufuli hajazungumzia chochote kuhusu agizo hilo la Waziri wa habari Dkt. Harison Mwakyembe.

Vilevie Dkt. Abbas amesema kuwa Umma unakumbushwa kuwa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015 kinakataza na kutoa adhabu kali ikiwemo kifungo jela kwa wanaoeneza taarifa za uongo

Hata hivyo, amesisitiza kuwa mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika vizuri ili kuweza kupeleka ujumbe uliojitoshereza kwa jamii na uzushi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu