Serikali yaonyesha dhamira kutumia lugha ya kiswahili

Serikali ina dhamira ya dhati katika kuendeleza na kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Aidha, walimu na wataalamu wa lugha ya Kiswahili nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kukua kwa lugha hiyo katika nchi zinazohitaji wataalamu wa lugha hiyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili, kwenye ukumbi wa Bunge  Mjini Dodoma.

Amesema katika kuendeleza na kukitumia Kiswahili, serikali imekusudia kuwa na miundombinu imara ya kuwezesha upatikanaji wa wakalimani, walimu wa Kiswahili kwa wageni na wafasiri wa kutosha kukidhi mahitaji yanayoongezeka kwa kasi.

Katibu Mtendaji wa BAKITA, Dk Seleman Sewangi alisema baraza limefikia hatua hiyo baada ya kuwapo kwa hazina ya misamiati mipya iliyofanyiwa utafiti.

Kamusi Kuu ya Kiswahili imeandaliwa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na kampuni ya uchapishaji ya Longhom ya Kenya.

Exit mobile version