Serikali imesema itapeleka bungeni marekebisho ya Sheria ya
Vyama vya Siasa, ili kuvilazimisha kuwa na sera itakayoweka
mwongozo wa kujumuisha wanawake katika kuwania nagasi
mbali mbali za uongozi.
Hayo yameeleza leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri
katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Ummy
Ndeliananga,wakati akijibu maswali ya nyongeza ya mbunge wa
Viti maalum Anatropia Theonest.
Katika swali lake la msingi mbunge huyo alihoji ni wanawake
wangapi wamekuwa wabunge wa majimbo na madiwani katika
chaguzi tatu mfululizo zilizopita.
