Serikali yatangaza punguzo kubwa la bei za dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara baada ya kuanza utaratibu wa bohari kuu ya dawa kununua dawa moja kwa moja kutoka viwandani badala ya kupitia kwa mawakala.
Akitangaza utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanayolenga kuunga mkono jitihada zake katika kujenga uchumi wa viwanda bohari kuu ya dawa kununua dawa zenye ubora kutoka kwa wazalishaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema gharama za kununua dawa zitapungua kwa asilimia 15 hadi 80 ikiwemo dawa ya chanjo ya homa ya ini.
Aidha,Mh. Ummy Mwalimu licha ya kuziagiza halmashauri zahanati vituo vya afya hospitali za serikali kutumia bei elekezi ya dawa zilizotolewa na wizara ya afya kupitia orodha ya bei kwa bohari kuu ya dawa MSD tayari amesema serikali imeingia mikataba na wazalishaji 73.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa bohari kuu ya dawa MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu amekabidhi kitabu kipya cha bei za dawa zenye punguzo ambazo mabadiliko ya bei yameanza kutumika julai mosi mwaka huu na kuwakikishia wananchi kuwa watafuata maelekezo ya serikali kama ilivyoagiza.
