Serikali yatoa kauli juu ya thamani ya Shilingi.

 

Bunge limeelezwa kuwa kushuka au kupanda kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania, hakutokani na kuruhusu bidhaa na huduma kutozwa kwa Dola, bali kunatokana na misingi ya shughuli za kiuchumi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashantu Kijaji, ametoa kauli hiyo bungeni akijibu swali la mbunge wa Viwawa CCM Japhet Hasunga.

Mbunge huyo alitaka kujua hatua ambazo Serikali inatarajia kuchukua, ili kuimarisha Shilingi ya Tanzania na kupiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini.

Naibu waziri alitaja sababu za kushuka kwa thamani ya Shilingi Tanzania, kuwa ni nakisi ya urari wa biashara ya nje ya nchi ambayo husababisha sarafu ya Tanzania kushuka thamani kama mauzo ya bidhaa ya nje.

Dk Kijaji amesema sababu nyingine ni tofauti ya misimu ya upatikanaji wa fedha za kigeni, kutokana na biashara za msimu kusababisha kuserereka kwa Shilingi.

Naibu waziri alitoa mfano wa Afrika Kusini akisema pamoja na sheria ya kutokutumia.

Exit mobile version