Serikali yatoa siku 7 kawa Halmashauri ambazo hazijakamilisha manunuzi ya dawa na vifaa tiba.

In Kitaifa

Serikali imetoa siku saba kwa halmashauri ambazo hazijamaliza matumizi ya fedha hasa kwa upande wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba, kutoa maelezo kwa njia ya maandishi ni kwanini fedha hizo hazijatumika kama zilivyopangwa wakati wananchi wakilalamika kukosa dawa na kwanini wasichukuliwe hatua.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya uliomalizika mjini hapa.

Agizo hili linawahusu Makatibu Tawala wa Wilaya na Mikoa yote hapa nchini ambapo,amesema hali ya matumizi ya fedha katika halmashauri nyingi ni changamoto kubwa kwani licha ya wananchi kukosa dawa na vifaa tiba bado kuna halmashauri zina fedha nyingi kwenye akaunti zao na kuvuka mwaka wa fedha na wakiwa na bakaa.

Waziri huyo amesema si lengo la serikali kuwepo na fedha zinazovuka mwaka, hasa ikizingatiwa kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 fedha za mfuko wa pamoja wa Afya, (HBF) zilifika kwenye mikoa na halmashauri kwa wakati lakini bado wananchi hawana dawa na vifaa tiba.

Amewaagiza makatibu tawala wa mikoa yote 26 kwamba halmashauri zote ambazo hazijamaliza matumizi ya fedha hasa upande wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba zitoe maelezo.

Simbachawene amesema mwaka 2015/16 fedha hizo zilitolewa bila kujali matokeo kwa nia ya kuzitaka halmashauri kutumia fedha hizo kuboresha huduma kabla hazijaanza kupimwa kwa matokeo, isipokuwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia zilitolewa kwa njia ya matokeo kwa kutumia utaratibu huo.

Hata hivyo, amesema serikali kwa kushirikiana na wadau, wameamua kuanzia mwaka huu wa fedha 2017/18, serikali itaanza kupeleka moja kwa moja kwenye akaunti za vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni katika hatua ya kuimarisha huduma za afya ngazi za msingi na kudhibiti upotevu na uchelewaji wa fedha kuwafikia watoa huduma.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu