Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi, imetoa ufafanuzi kuhusu suala la faida na mgao wa asilimia 50/50 na kusema jambo hilo limekuwa halifahamiki vizuri kwa watu wengi.
Profesa Kabudi amesema kuwa serikali ya Tanzania itapata asilimia 16 ambazo zinapatikana bila malipo kwa mujibu wa sheria za madini, kama ambavyo zimepitishwa huku Barrick wao wakibaki na asilimi 84.
Antenna imemnasa Prof Palamagamba Kabudi,akilifafanua hilo kwa uzuri, baada ya kuonekana kuwachanganya wengi baada ya taarifa aliyokabidhiwa jana mheshimiwa raisa Magufuli.
