Serikali za Uingereza na Marekani, zatoa msaada wa Euro milioni 40.4 sawa na (Sh bilioni 101) kwa Serikali ya awamu ya tano.

In Kitaifa

Jumuiya ya kimataifa imeendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika hatua zake za kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo Umoja wa Ulaya (EU), Serikali za Uingereza na Marekani, kwa pamoja, zimetoa msaada wa Euro milioni 40.4 sawa na  (Sh bilioni 101).

Fedha hizo ni kwa ajili ya kufadhili ujenzi wa barabara kuanzia Kidatu-Ifakara mkoani Morogoro, itakayojengwa kwa kiwango cha lami.

Kupatikana kwa fedha hizo, mbele ya uwakilishi wa EU, Wizara ya Fedha na Mipango imetiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds, kandarasi ya ujenzi wa barabara hiyo, yenye urefu wa kilometa 67.

Mkataba huo umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaaban, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Dan Yzhak Shahn, ambaye ni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds.

Kiasi hicho cha fedha ni sawa na Euro milioni 40.4 ambapo Euro milioni 29.6 zimetolewa kwa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Shirika la Misaada la Uingereza (UKAID), huku kiasi kinachobaki cha Euro milioni 10.8 kikitolewa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).

Akizungumza  mara baada ya kutiwa saini kwa kandarasi hiyo, Naibu Katibu Mkuu amesema ujenzi wa barabara hiyo utakaohusisha pia ujenzi wa daraja la Mto Ruaha Mkuu, utasaidia wakulima wadogo kupitia Programu ya Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), walioko katika Bonde la Mto Kilombero, kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu