Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir amesisitiza haja ya waumini wa madhehebu mbalimbali za dini hapa nchini kushikamana zaidi, ili kulinda na kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa uliopo nchini.

Mufti Abubakar Zubeir ametoa msisitizo huo jijini Dar es salaam katika hafla ya futari iliyowakutanisha waumini wa madhehebu tofauti ya dini, iliyoandaliwa kwa pamoja na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA kwa kushirikiana na Jumuiya ya ‘Khoja Shia Ithnaasheri’ mkoani Dar es salaam.
Amesema kwa mujibu wa mafundisho ya vitabu vyote vya dini, binadamu wote ni ndugu kwa sababu wanatokana na asili moja, licha ya binadamu hao kuwa na dini na madhehebu tofauti.
Hafla hiyo iliyopewa jina la ‘Interfaith Iftar’ ilihudhuriwa na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini wakiwemo viongozi wa kisiasa na mabalozi.
Exit mobile version